Tafuta kozi au mtoaji wake


Toleo la PDF la ukurasa huu (10kb)

Tazama mwongozo wa kozi na watoaji katika kila mkoa:

Mwongozo wa kitaifa

Aina kuu za watoaji wa elimu ya jumuia zimeelezwa hapa chini, pamoja na mashirika yanayohusiana ya kitaifa.

Vyuo vya kijamii

Vyuo vya kijamii ni watoaji wakuu wa elimu ya jamii, hasa katika New South Wales, Victoria na ACT. Shirika lao mlezi ni Community Colleges Australia.

http://www.cca.edu.au

Nyumba za jumuia na vituo vya kusomea vya jamii

Vituo hivi vinavyosimamiwa na mashirika ya jamii ya asili vinatoa shughuli mbalimbali za jamii, elimu na michezo katika kukaribisha, mazingira ya kusaidia. Shirika laThe Australian Neighbourhood Houses and Centres Association linawakilisha zaidi ya mashirika 1,000 kitaifa.

http://www.anhlc.asn.au/about-anhca

TAFE

Institutes of Technical and Further Education (TAFE) inatoa mafunzo ya ufundi yanayojulikana (kuelekea kwenye elimu inayotambulika) pamoja na kozi nyingi za mda mfupi. Mwongozo wa maelekezo ya TAFE unapatikana chini ya kila mkoa.

Kozi za kusoma na kuhesabu

Mashirika ya mkoa ya elimu ya kusoma na kuhesabu ya watu wazima inatoa habari za kozi katika kila mkoa. Shirika mama la taifa ni Australian Council for Adult Literacy.

http://www.acal.edu.au

Maktaba

Maktaba za jamii zinatoa shughuli mbalimbali za elimu kqwa wakazi wa eneo. Mtandao wa The Australian Libraries Gateway unakuruhusu kutafuta maktaba katika eneo lako.

http://www.nla.gov.au/apps/libraries?action=LibSearch

Vituo vya habari vya wahamiajii

MVituo vya habari vya wahamiaji vinatoa msaada wa huduma kwa wahamiaji na wakimbizi, ikijumuisha lugha ya Kiingereza na kozi zingine. Shirika mama la mashirika yanayofanya kazi na wakimbizi na watafuta ukimbizi ni Refugee Council of Australia.

http://www.refugeecouncil.org.au

Chuo kikuu cha kizazi cha tatu (U3A)

U3A ni harambee ya kimataifa ambayo inawahimiza watu wa zaidi ya miaka 50 ambao hawajaajiriwa mda wote kuhusika katika shughuli mbalimbali za kimaisha. Tovuti inajumisha mwongozo wa vikundi vya asili vya U3A .

http://www.u3aonline.org.au

Mafunzo ya Ukubwani ya Australia (Adult Learning Australia)

Adult Learning Australia (ALA) ni shirika mama la kitaifa kwa mafunzo ya ukubwani.

http://www.ala.asn.au

Kozi nchini Australia

Hii tovuti ya kibiashara inaorodhesha kozi zote za TAFE na chuo kikuu na inatoa mwongozo wa zaidi ya kozi 10,000.

http://www.courses.com.au