Utangulizi

You are missing some Flash content that should appear here! Perhaps your browser cannot display it, or maybe it did not initialize correctly.

Toleo la PDF la ukurasa huu (6kb)

Wiki ya Wanafunzi wakubwa inasherekea utajiri wa nafasi za masomo ya watu wazima yaliyopo nchini Australia.

Elimu ya jamii iko wazi kwa watu wa miaka yote na asili ya hitimu tofauti . Kila mwaka mamia ya maelfu ya wanaaustralia wanasoma ujuzi wa ufundi, kilimo, biashara, kompyuta, sanaa na ufundi, muziki, afya, kupika na lugha mbalimbali kupitia watoaji wa elimu za jamii.

Elimu ya jamii na nafuu na inatolewa katika mazingira ya urafiki, ikijumuisha vyuo, nyumba za jamii, maktaba na TAFE. Baadhi ya vituo vya habari vya wahamiaji vinatoa kozi za elimu, na wanaweza pia kukusaidia kukutafutia kozi inayoendana na mahitaji yako. Unaweza kujiunga na vikundi vya shughuli vya kawaida, semina ya siku moja, au kozi ya wiki kadhaa au miezi kadhaa.

Kozi za elimu ya jamii ambazo hazijasajiliwa (kozi ambazo hazipelekei elimu inayojulikana) zinaweza kusaidia kukuandaa kwa elimu ya juu, ajira, au kubadilisha kazi. Kozi fupi inaweza kukusaidia kupata ufundi mpya au utaalamu mpya, kupanua matakwa binafsi, kuongeza uwezo wa kuwasiliana, na kukutana na watu katika jamii yako. Utaweza kuelewa vizuri mwongozo wa elimu ya Australia na kukufanya kujiamini kupata hatua mpya katika kazi au masomo.

Kila la heri katika safari yako ya kujifunza maishani!